Job 2:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Marafiki watatu wa Yobu: Elifazi kutoka Temani, Bildadi kutoka Shua na Sofari kutoka Naamathi, walisikia juu ya maafa yote yaliyompata Yobu. Basi, wakaamua kwa pamoja waende kumpa pole na kumfariji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi rafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia kuhusu taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga kutoka nyumbani mwao, wakakutana ili kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikawa hao rafikize Ayubu watatu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikilia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumlilia Ayubu na kumtuliza moyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Marafiki watatu wa Yobu: Elifazi kutoka Temani, Bildadi kutoka Shua na Sofari kutoka Naamathi, walisikia juu ya maafa yote yaliyompata Yobu. Basi, wakaamua kwa pamoja waende kumpa pole na kumfariji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi marafiki watatu wa Ayubu, Elifazi, Mtemani na Bildadi, Mshuhi na Sofari, Mnaamathi waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka majumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi marafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka manyumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikawa hao marafiki watatu wa Ayubu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumfariji Ayubu na kumtuliza moyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Marafiki watatu wa Yobu: Elifazi kutoka Temani, Bildadi kutoka Shua na Sofari kutoka Naamathi, walisikia juu ya maafa yote yaliyompata Yobu. Basi, wakaamua kwa pamoja waende kumpa pole na kumfariji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Rafiki zake Iyobu watatu walipoyasikia hayo mabaya yote yaliyompata, ndipo, walipoondoka kila mtu mahali pake, Elifazi wa Temani na Bildadi wa Sua na Sofari wa Nama, wakapatana kwenda pamoja kumpongeza na kumtuliza moyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikawa hao rafikize Ayubu watatu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikilia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumlilia Ayubu na kumtuliza moyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Warafiki watatu wa Yobu walisikia juu ya hasara zote zilizomupata Yobu, wakaamua kwa pamoja waende kumupa pole na kumufariji. Majina yao ni: Elifasi kutoka inchi ya Temani, Bildadi wa inchi ya Suhi na Zofari wa inchi ya Namati.