Job 2:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Shetani akaondoka mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamtesa Yobu kwa madonda mabaya tangu wayo wa mguu wake mpaka utosini mwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Shetani akatoka mbele za Mwenyezi Mungu, naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Shetani akaondoka mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamtesa Yobu kwa madonda mabaya tangu wayo wa mguu wake mpaka utosini mwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Shetani akatoka mbele za BWANA naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Shetani akatoka mbele za bwana naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hadi utosi wa kichwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Shetani akaondoka mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamtesa Yobu kwa madonda mabaya tangu wayo wa mguu wake mpaka utosini mwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Satani alipotoka usoni pake Bwana, akampiga Iyobu na kumwuguza majipu mabaya kutoka kwenye wayo hata utosini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Shetani akaondoka mbele ya Yawe, akamutesa Yobu kwa vidonda vikali tangia kwenye miguu yake mpaka kwenye kichwa chake.