Job 28:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Binadamu huchimba mashimo mbali na makazi ya watu, mbali na watu mahali kusipofikika, wachimba madini huninginia wamefungwa kamba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; mbali na wanadamu huning’inia na kubembea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning'inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Binadamu huchimba mashimo mbali na makazi ya watu, mbali na watu mahali kusipofikika, wachimba madini huning'inia wamefungwa kamba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu, mbali na wanadamu huning'inia na kupembea kwa kamba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; mbali na wanadamu huning’inia na kupembea kwa kamba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning'inia mbali na watu, huyumbayumba huku na huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Binadamu huchimba mashimo mbali na makazi ya watu, mbali na watu mahali kusipofikika, wachimba madini huninginia wamefungwa kamba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko anachimbua shimo refu sana, kisha nayo njia ya ndani ya nchi pasipokaa watu; wanawahauliwa kwa kuwa chini ya hapo, watu wanapokanyaga; ndiko, wanakojiangika na kuning'inia, watu wengine wakiwa mbali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning’inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanadamu anachimba mashimo mbali na makao ya watu, mbali na watu pahali kusipofikiwa, wachimba madini wananinginia wakifungwa kamba.