Job 30:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini sasa watu wananidhihaki, tena watu walio wadogo kuliko mimi; watu ambao baba zao niliwaona hawafai hata kuwaangalia mbwa wangu wakilinda kondoo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuliko mimi wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha, Ambao baba zao niliwadharau hata kuwaweka na mbwa wa kundi langu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini sasa watu wananidhihaki, tena watu walio wadogo kuliko mimi; watu ambao baba zao niliwaona hawafai hata kuwaangalia mbwa wangu wakilinda kondoo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuliko mimi wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha, Ambao baba zao ningewadharau hata kuwasimamia mbwa wa kundi langu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini sasa watu wananidhihaki, tena watu walio wadogo kuliko mimi; watu ambao baba zao niliwaona hawafai hata kuwaangalia mbwa wangu wakilinda kondoo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa wananicheka walio wenye siku chache kuliko mimi, ambao baba zao nilikataa kuwaweka mahali, mbwa wa makundi yangu ya kondoo walipokuwa nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha, Ambao baba zao niliwadharau hata kuwaweka na mbwa wa kundi langu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa watu wananichekelea, tena watu wanaokuwa wadogo kuliko mimi; watu ambao niliwaona baba zao hawafai hata kuwahesabu kama imbwa wangu wakilinda kondoo.