Job 37:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo sauti yake hunguruma, sauti ya Mungu hunguruma kwa fahari na muda huo wote umeme humulikamulika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake; Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. Wakati sauti yake inanguruma tena, huuachilia umeme wake wa radi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo sauti yake hunguruma, sauti ya Mungu hunguruma kwa fahari na muda huo wote umeme humulikamulika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake, Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. Wakati sauti yake ingurumapo tena, huuachilia umeme wake wa radi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake; Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. Wakati sauti yake ingurumapo tena, huuachilia umeme wake wa radi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo sauti yake hunguruma, sauti ya Mungu hunguruma kwa fahari na muda huo wote umeme humulikamulika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauti yake hunguruma, ukiisha kuwapo; ndipo, unapoivumisha hiyo sauti yake yenye utukufu; kusudi sauti yake ipate kusikilika, hauzuii umeme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu sauti yake inanguruma, sauti ya Mungu inanguruma kwa utukufu; yeye hazuizi umeme wakati inaposikilika.