Job 42:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya Yobu kuwaombea rafiki zake, Mwenyezi-Mungu akamrudishia Yobu hali yake ya kwanza. Alimpa maradufu ya yote aliyokuwa nayo hapo awali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, Mwenyezi Mungu akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya Yobu kuwaombea rafiki zake, Mwenyezi-Mungu akamrudishia Yobu hali yake ya kwanza. Alimpa maradufu ya yote aliyokuwa nayo hapo awali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, BWANA akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo kabla.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, bwana akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha BWANA akamrejeshea Ayubu mali yake, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya Yobu kuwaombea rafiki zake, Mwenyezi-Mungu akamrudishia Yobu hali yake ya kwanza. Alimpa maradufu ya yote aliyokuwa nayo hapo awali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Bwana akayafungua mafungo ya Iyobu, alipowaombea wenzake; nayo yote, Iyobu aliyokuwa nayo, Bwana akayarudisha na kuyaongeza, akayapata yale ya kale mara mbili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya Yobu kuwaombea warafiki zake, Yawe akamurudishia Yobu hali yake ya kwanza. Akamupa mara mbili ya yote aliyokuwa nayo pale mbele.