Job 42:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha ndugu zake, dada zake na rafiki wote waliomfahamu hapo awali wakamwendea nyumbani kwake, wakala chakula pamoja naye. Wakampa pole na kumfariji kwa ajili ya mateso yote ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemletea. Kila mmoja wao akampa Yobu fedha na pete ya dhahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo ndugu zake na dada zake wote, na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni wakaja, wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote Mwenyezi Mungu aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha ndugu zake, dada zake na rafiki wote waliomfahamu hapo awali wakamwendea nyumbani kwake, wakala chakula pamoja naye. Wakampa pole na kumfariji kwa ajili ya mateso yote ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemletea. Kila mmoja wao akampa Yobu fedha na pete ya dhahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu kabla, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote BWANA aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote bwana aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wakamwendea ndugu zake wote, wanaume kwa wanawake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakampa pole na kumliwaza kwa ajili ya mateso hayo yote aliyoleta BWANA juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha ndugu zake, dada zake na rafiki wote waliomfahamu hapo awali wakamwendea nyumbani kwake, wakala chakula pamoja naye. Wakampa pole na kumfariji kwa ajili ya mateso yote ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemletea. Kila mmoja wao akampa Yobu fedha na pete ya dhahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaja kwake ndugu zake wote wa kiume na wa kike nao waliojuana naye kale, wakala naye chakula nyumbani mwake, wakampongeza na kumtuliza moyo kwa ajili ya hayo mabaya yote, Bwana aliyokuwa alimletea, wakampa kila mtu kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote BWANA aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha wandugu zake, wadada zake na warafiki wote waliomufahamu mbele wakamwendea kwake, wakakula chakula pamoja naye. Wakamupa pole na kumufariji kwa ajili ya mateso yote ambayo Yawe alikuwa amemuletea. Kila mumoja wao akamupa Yobu feza na pete ya zahabu.