Job 42:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu alipomaliza kuongea na Yobu, alimwambia Elifazi, Mtemani, “Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na marafiki zako wawili kwani hamkusema ukweli juu yangu kama mtumishi wangu Yobu alivyofanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Mwenyezi Mungu kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira nawe na rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kunihusu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu alipomaliza kuongea na Yobu, alimwambia Elifazi, Mtemani, “Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na marafiki zako wawili kwani hamkusema ukweli juu yangu kama mtumishi wangu Yobu alivyofanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya BWANA kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi, Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya bwana kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu alipomaliza kuongea na Yobu, alimwambia Elifazi, Mtemani, “Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na marafiki zako wawili kwani hamkusema ukweli juu yangu kama mtumishi wangu Yobu alivyofanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Bwana alipokwisha kumwambia Iyobu maneno haya, Bwana akamwambia Elifazi wa Temani: Makali yangu yamekuwakia wewe na wenzako hawa wawili, kwani maneno, mliyoyasema kuwa yangu, hayakunyoka kama yale ya mtumishi wangu Iyobu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe alipomaliza kuongea na Yobu, akamwambia Elifasi wa inchi ya Temani: “Kasirani yangu imewaka juu yako na warafiki zako wawili maana hamukusema ukweli juu yangu kama vile mutumishi wangu Yobu alivyofanya.