Joel 1:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mizabibu imenyauka; mitini imedhoofika; mikomamanga, mitende na mitofaa imekauka, naam miti yote shambani imekauka. Furaha imetoweka miongoni mwa watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mzabibu umekauka na mtini umenyauka; mkomamanga, mtende na mtofaa, miti yote shambani, imekauka. Hakika furaha yote ya mwanadamu imeondoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba imekauka; Maana furaha imekauka katika wanadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mizabibu imenyauka; mitini imedhoofika; mikomamanga, mitende na mitofaa imekauka, naam miti yote shambani imekauka. Furaha imetoweka miongoni mwa watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mzabibu umekauka na mtini umenyauka; mkomamanga, mtende na mtofaa, miti yote ya shambani, imekauka. Hakika furaha yote ya mwanadamu imeondoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mzabibu umekauka na mtini umenyauka; mkomamanga, mtende na mtofaa, miti yote shambani, imekauka. Hakika furaha yote ya mwanadamu imeondoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba imekauka; Maana furaha imetoweka kwa wanadamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mizabibu imenyauka; mitini imedhoofika; mikomamanga, mitende na mitofaa imekauka, naam miti yote shambani imekauka. Furaha imetoweka miongoni mwa watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mizabibu imekauka, mikuyu imefifia, mikomamanga na mitende na michungwa, miti yote pia ya shambani imekauka, kweli nazo furaha zimekaukiana, zimewapotelea watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba imekauka; Maana furaha imekauka katika wanadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mizabibu imenyauka, mitini imekauka, miti yote ya matunda imekauka. Furaha imetoweka kati ya watu.