Joel 1:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini. Kusanyeni wazee na wakazi wote wa nchi, nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na humo mkamlilie Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tangazeni saumu takatifu; liiteni kusanyiko takatifu. Waiteni wazee na wote wanaoishi katika nchi waende katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, wakamlilie Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa Bwana, Mungu wenu, Na kumlilia Bwana,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini. Kusanyeni wazee na wakazi wote wa nchi, nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na humo mkamlilie Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tangazeni saumu takatifu; liiteni kusanyiko takatifu. Iteni wazee na wote waishio katika nchi waende katika nyumba ya BWANA Mungu wenu, wakamlilie BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tangazeni saumu takatifu; liiteni kusanyiko takatifu. Iteni wazee na wote waishio katika nchi waende katika nyumba ya bwana Mwenyezi Mungu wenu, wakamlilie bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini. Kusanyeni wazee na wakazi wote wa nchi, nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na humo mkamlilie Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Eueni mfungo! Utangazeni mkutano! Wakusanyeni wazee nao wote wanaokaa katika nchi hii, waje Nyumbani mwa Bwana Mungu wenu, mmlalamikie Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutoe amri watu wafunge kula chakula; muwaalike watu kuja kwa mukutano wa kidini. Mukusanye wazee na wakaaji wote wa inchi, katika nyumba ya Yawe, Mungu wenu, na mule mumulilie Yawe.