Joel 1:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mbegu zinaoza udongoni; ghala za nafaka ni ukiwa mtupu, ghala zimeharibika, kwa kukosa nafaka ya kuhifadhi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mbegu zinakauka chini ya mabonge ya udongo. Maghala yameachwa katika uharibifu, maghala ya nafaka yamebomolewa, kwa maana hakuna nafaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika; kwa maana nafaka imekauka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mbegu zinaoza udongoni; ghala za nafaka ni ukiwa mtupu, ghala zimeharibika, kwa kukosa nafaka ya kuhifadhi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mbegu zinakauka chini ya mabonge ya udongo. Ghala zimeachwa katika uharibifu, ghala za nafaka zimebomolewa, kwa maana hakuna nafaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mbegu zinakauka chini ya mabonge ya udongo. Ghala zimeachwa katika uharibifu, ghala za nafaka zimebomolewa, kwa maana hakuna nafaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; mabohari yameachwa ukiwa; ghala zimeharibika; kwa maana nafaka imekauka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mbegu zinaoza udongoni; ghala za nafaka ni ukiwa mtupu, ghala zimeharibika, kwa kukosa nafaka ya kuhifadhi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mbegu zimenyauka chini ya madongo yao, vilimbiko vimetoweka, vyanja vimebomolewa, kwani ngano zimekauka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika; kwa maana nafaka imekauka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbegu zinaoza ndani ya udongo; gala zimebaki bila kitu, vibanda vya kuwekea mavuno vimebomoka, kwa maana hakuna tena ngano.