Joel 2:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msirarue mavazi yenu kuonesha huzuni bali nirudieni kwa moyo wa toba.” Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; yeye amejaa neema na huruma; hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili; daima yu tayari kuacha kuadhibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Rarueni mioyo yenu na siyo mavazi yenu. Mrudieni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, huona huruma, hujizuia kuleta maafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msirarue mavazi yenu kuonesha huzuni bali nirudieni kwa moyo wa toba.” Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; yeye amejaa neema na huruma; hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili; daima yu tayari kuacha kuadhibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Rarueni mioyo yenu na siyo mavazi yenu. Mrudieni BWANA, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, huona huruma, hujizuia kuleta maafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Rarueni mioyo yenu na siyo mavazi yenu. Mrudieni bwana, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, huona huruma, hujizuia kuleta maafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msirarue mavazi yenu kuonesha huzuni bali nirudieni kwa moyo wa toba.” Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; yeye amejaa neema na huruma; hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili; daima yu tayari kuacha kuadhibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Irarueni mioyo yenu, msiyararue mavazi yenu! Kisha rudini kwa Bwana Mungu wenu! Kwani Yeye ni mwenye utu na huruma, tena mwenye uvumilivu na upole mwingi; hugeuza moyo, asifanye mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munapasua nguo zenu kwa kuonyesha huzuni, lakini inafaa mioyo yenu ipasuke vilevile. Murudilie Yawe, Mungu wenu. Yeye amejaa huruma na rehema, hakasiriki upesi, ni mwingi wa wema, na tayari kubadilisha nia zake kusudi asiazibu.