Joel 2:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atabadili nia na kuwapeni baraka ya mazao, mkamtolea sadaka za nafaka na kinywaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma na kuacha baraka nyuma yake: sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
N'nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atabadili nia na kuwapeni baraka ya mazao, mkamtolea sadaka za nafaka na kinywaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma na kuacha baraka nyuma yake: sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji kwa ajili ya BWANA Mungu wenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma na kuacha baraka nyuma yake: sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji kwa ajili ya bwana Mwenyezi Mungu wenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atabadili nia na kuwapeni baraka ya mazao, mkamtolea sadaka za nafaka na kinywaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Labda atageuza moyo tena, atuachilie mbaraka atakapoondoka, akiwapatia vilaji na vinywaji vya kumtambikia Bwana mungu wenu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
N’nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Labda Yawe, Mungu wenu, atabadilisha nia na kuwapa baraka ya mazao, mutaweza kumutolea sadaka za chakula na kinywaji.