Joel 2:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kati ya madhabahu na lango la hekalu, makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu, walie na kuomba wakisema: “Wahurumie watu wako, ee Mwenyezi-Mungu. Usiyaache mataifa mengine yatudharau na kutudhihaki yakisema, ‘Yuko wapi basi Mungu wao?’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makuhani, ambao wanahudumu mbele za Mwenyezi Mungu, na walie katikati ya ukumbi wa Hekalu na madhabahu. Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee Mwenyezi Mungu. Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa, neno la dhihaka kati ya mataifa. Kwa nini wasemezane miongoni mwao, ‘Yuko wapi Mungu wao?’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kati ya madhabahu na lango la hekalu, makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu, walie na kuomba wakisema: “Wahurumie watu wako, ee Mwenyezi-Mungu. Usiyaache mataifa mengine yatudharau na kutudhihaki yakisema, ‘Yuko wapi basi Mungu wao?’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makuhani, ambao wanahudumu mbele za BWANA, na walie katikati ya ukumbi wa Hekalu na madhabahu. Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee BWANA. Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa, neno la dhihaka kati ya mataifa. Kwa nini wasemezane miongoni mwao, ‘Yuko wapi Mungu wao?’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makuhani, ambao wanahudumu mbele za bwana, na walie katikati ya ukumbi wa Hekalu na madhabahu. Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee bwana. Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa, neno la dhihaka kati ya mataifa. Kwa nini wasemezane miongoni mwao, ‘Yuko wapi Mungu wao?’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee BWANA, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwa nini waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kati ya madhabahu na lango la hekalu, makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu, walie na kuomba wakisema: “Wahurumie watu wako, ee Mwenyezi-Mungu. Usiyaache mataifa mengine yatudharau na kutudhihaki yakisema, ‘Yuko wapi basi Mungu wao?’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watambikaji wanaomtumikia Bwana na walie katikati ya ukumbi na meza ya kutambikia, waseme: Bwana, wahurumie walio ukoo wako! Usiwatoe walio fungu lako, watukanwe, wamizimu wakiwatawala! Mbona wataka, waseme kwa makabila mengine: Mungu wao yuko wapi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee BWANA, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati ya mazabahu na mulango wa hekalu, makuhani wanaomutumikia Yawe, walie na kuomba wakisema: Uwahurumie watu wako, ee Yawe. Usiyaache mataifa mengine yatuzarau na kutuchekelea yakisema: Yuko wapi basi Mungu wao?