Joel 2:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Furahini, enyi watu wa Siyoni, shangilieni kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, maana amewapeni mvua za masika, amewapeni mvua ya kutosha: Mvua za masika na mvua za vuli kama hapo awali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Furahini, enyi watu wa Sayuni, shangilieni katika Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa kuwa amewapa mvua za vuli kwa kipimo cha haki. Anawapelekea mvua nyingi, mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Furahini, enyi watu wa Siyoni, shangilieni kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, maana amewapeni mvua za masika, amewapeni mvua ya kutosha: mvua za masika na mvua za vuli kama hapo awali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Furahini, Enyi watu wa Sayuni, shangilieni katika BWANA Mungu wenu, kwa kuwa amewapa mvua za vuli kwa kipimo cha haki. Anawapelekea mvua nyingi, mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Furahini, enyi watu wa Sayuni, shangilieni katika bwana Mwenyezi Mungu wenu, kwa kuwa amewapa mvua za vuli kwa kipimo cha haki. Anawapelekea mvua nyingi, mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama awali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Furahini, enyi watu wa Siyoni, shangilieni kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, maana amewapeni mvua za masika, amewapeni mvua ya kutosha: Mvua za masika na mvua za vuli kama hapo awali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Sioni, shangilieni! Mfurahieni Bwana Mungu wenu! Kwani anawapa mvua ya masika hapo ipasapo, anawanyeshea kwanza mvua za masika nazo za vuli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufurahi, enyi watu wa Sayuni, mushangilie kwa sababu ya Yawe, Mungu wenu, maana amewapa mvua zinazowafalia, amewapa mvua ya kutosha: mvua za kwanza na mvua za katikati kama pale mbele.