Joel 2:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtapata chakula kingi na kutosheka; mtalisifu jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu. Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtakuwa na wingi wa vyakula hadi mshibe, na mtalisifu jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu; kamwe watu wangu hawataaibishwa tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtapata chakula kingi na kutosheka; mtalisifu jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu. Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe, na mtalisifu jina la BWANA Mungu wenu, ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu; kamwe watu wangu hawataaibishwa tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe, na mtalisifu jina la bwana Mwenyezi Mungu wenu, ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu; kamwe watu wangu hawataaibishwa tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtapata chakula kingi na kutosheka; mtalisifu jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu. Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtakula kabisa na kushiba, mlisifu Jina la Bwana Mungu wenu, kwa kuwa alifanya kwenu mataajabu! Kweli walio ukoo wangu hawatapatwa na soni kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutapata chakula kingi na kutosheka; mutalisifu jina la Yawe, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu. Watu wangu, hawatazarauliwa tena hata kidogo.