Joel 2:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtatambua kwamba mimi nimo miongoni mwenu, enyi Waisraeli; kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, ndimi Mungu wenu wala hakuna mwingine. Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo mtajua kuwa mimi niko katika Israeli, kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kwamba hakuna mwingine; kamwe watu wangu hawataaibika tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtatambua kwamba mimi nimo miongoni mwenu, enyi Waisraeli; kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, ndimi Mungu wenu wala hakuna mwingine. Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo mtakapojua kwamba mimi niko katika Israeli kwamba mimi ndimi BWANA Mungu wenu, na kwamba hakuna mwingine; kamwe watu wangu hawataaibika tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo mtakapojua kwamba mimi niko katika Israeli kwamba mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu, na kwamba hakuna mwingine; kamwe watu wangu hawataaibika tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtatambua kwamba mimi nimo miongoni mwenu, enyi Waisraeli; kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, ndimi Mungu wenu wala hakuna mwingine. Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi niko katikati ya Waisiraeli, ya kuwa mimi Bwana ni Mungu wenu, siye mwingine. Kweli walio ukoo wangu hawatapatwa na soni kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutatambua kwamba mimi niko kati yenu, enyi Waisraeli; na kwamba mimi Yawe, ndimi Mungu wenu wala hakuna mwingine. Watu wangu, hawatazarauliwa tena hata kidogo.