Joel 3:12 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Haya mataifa na yajiweke tayari; yaje kwenye bonde liitwalo: ‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu’. Huko, mimi Mwenyezi-Mungu, nitaketi kuyahukumu mataifa yote ya jirani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mataifa na yaamshwe; na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati, kwa kuwa nitaketi mahali pale kuhukumu mataifa yote yaliyo kila upande.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Haya mataifa na yajiweke tayari; yaje kwenye bonde liitwalo: ‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu’. Huko, mimi Mwenyezi-Mungu, nitaketi kuyahukumu mataifa yote ya jirani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mataifa na yaamshwe; na yasonge mbele kuelekea katika Bonde la Yehoshafati, kwa kuwa nitaketi mahali pale kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mataifa na yaamshwe; na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati, kwa kuwa nitaketi mahali pale kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafati; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Haya mataifa na yajiweke tayari; yaje kwenye bonde liitwalo: ‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu’. Huko, mimi Mwenyezi-Mungu, nitaketi kuyahukumu mataifa yote ya jirani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mataifa na waimbe, waje huko bondeni kwa Yosafati! Kwani ndiko, nitakakokaa, niwahukumu wao wa mataifa yote wakaao na kuwazunguka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.