Joel 3:16 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu ananguruma huko Siyoni; sauti yake inavuma kutoka Yerusalemu; mbingu na dunia vinatetemeka. Lakini Mwenyezi-Mungu ni kimbilio la watu wake, ni ngome ya usalama kwa Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu atanguruma kutoka Sayuni na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu; dunia na mbingu vitatikisika. Lakini Mwenyezi Mungu atakuwa kimbilio la watu wake, ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Bwana atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu ananguruma huko Siyoni; sauti yake inavuma kutoka Yerusalemu; mbingu na dunia vinatetemeka. Lakini Mwenyezi-Mungu ni kimbilio la watu wake, ni ngome ya usalama kwa Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA atanguruma kutoka Sayuni na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu; dunia na mbingu vitatikisika. Lakini BWANA atakuwa kimbilio la watu wake, ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana atanguruma kutoka Sayuni na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu; dunia na mbingu vitatikisika. Lakini bwana atakuwa kimbilio la watu wake, ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye BWANA atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini BWANA atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu ananguruma huko Siyoni; sauti yake inavuma kutoka Yerusalemu; mbingu na dunia vinatetemeka. Lakini Mwenyezi-Mungu ni kimbilio la watu wake, ni ngome ya usalama kwa Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana atakaponguruma mle Sioni, ataivumisha sauti yake mle Yerusalemu, mbingu na nchi zitetemeke. Lakini Bwana atakuwa kimbilio lao walio ukoo wake na ngome yao walio wana wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye BWANA atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini BWANA atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.