Joel 3:17 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hapo, ewe Israeli, utajua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, nakaa Siyoni, mlima wangu mtakatifu, Yerusalemu utakuwa mji mtakatifu; na wageni hawatapita tena humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ndipo mtajua kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Yerusalemu utakuwa mtakatifu; kamwe wageni hawatauvamia tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hapo, ewe Israeli, utajua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, nakaa Siyoni, mlima wangu mtakatifu, Yerusalemu utakuwa mji mtakatifu; na wageni hawatapita tena humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, BWANA Mungu wenu, nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Yerusalemu utakuwa mtakatifu; kamwe wageni hawataivamia tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, bwana Mwenyezi Mungu wenu, nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Yerusalemu utakuwa mtakatifu; kamwe wageni hawatavamia tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hapo, ewe Israeli, utajua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, nakaa Siyoni, mlima wangu mtakatifu, Yerusalemu utakuwa mji mtakatifu; na wageni hawatapita tena humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtakapojua, ya kuwa mimi Bwana ni Mungu wenu akaaye Sioni penye mlima wangu mtakatifu. Nao Yerusalemu utakuwa mji mtakatifu, msimopita wageni tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.