Joel 3:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mnataka kunifanya nini enyi Tiro na Sidoni na maeneo yote ya Filistia? Je, mna kisasi nami mnachotaka kulipiza? Kama mnalipiza kisasi, mimi nitawalipizeni mara moja!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, na ninyi ni kitu gani kwangu, enyi Tiro, na Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno lo lote? Upesi na kwa haraka nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mnataka kunifanya nini enyi Tiro na Sidoni na maeneo yote ya Filistia? Je, mna kisasi nami mnachotaka kulipiza? Kama mnalipiza kisasi, mimi nitawalipizeni mara moja!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa una nini dhidi yangu, Ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naam, na ninyi ni kitu gani kwangu, enyi Tiro, na Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno lolote? Upesi na kwa haraka nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mnataka kunifanya nini enyi Tiro na Sidoni na maeneo yote ya Filistia? Je, mna kisasi nami mnachotaka kulipiza? Kama mnalipiza kisasi, mimi nitawalipizeni mara moja!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi wa Tiro na wa Sidoni mwanitakiaje? Nanyi nyote mkaao upande wa Wafilisti? Je? Ninyi mwataka kunilipisha niliyofanyiziwa? Au mnacho, mtakacho kunifanyizia? Sasa hivi kwa upesi nitawarudishia matendo yenu, yaje kuwaangukia vichwani penu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, na ninyi ni kitu gani kwangu, enyi Tiro, na Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno lo lote? Upesi na kwa haraka nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa kama damu, mbele ya kutimia kwa siku ya Yawe, siku inayokuwa kubwa na ya kutisha.