John 1:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Neno alikuwako ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyo Neno alikuwako ulimwenguni, na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huyo Neno alikuwapo tayari ulimwenguni. Ulimwengu uliumbwa kupitia yeye, lakini ulimwengu haukumkubali.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Neno alikuwako ulimwenguni; na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Neno alikuwako ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyo Neno alikuwako ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kwa yeye, haukumtambua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyo Neno alikuwako ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Neno alikuwako ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ulikuwamo ulimwenguni, nao ulimwengu uliumbwa nao, lakini ulimwengu haukuutambua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Neno alikuwa yuko katika dunia, nayo dunia iliumbwa kwa njia yake, lakini ijapokuwa vile haikumutambua.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Alikuwako ulimwenguni, ulimwengu umepata kuwa kwa veye, wala ulimwengu haukumtambua.