John 1:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ambao walizaliwa si kwa maumbile ya kibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala mapenzi ya mtu, bali kutokana na Mungu mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa hawakuzaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali wamezaliwa kwa mapenzi ya Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, walikuwa watoto wa Mungu, lakini si kwa kuzaliwa kimwili. Haikuhusisha matamanio ya kibinadamu. Mungu mwenyewe aliwafanya kuwa watoto wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hawa wamekuwa watoto wa Mungu si kwa uwezo wa kibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali Mungu mwenyewe ndiye baba yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ambao walizaliwa si kwa maumbile ya kibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala mapenzi ya mtu, bali kutokana na Mungu mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio waliozaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio wasiozaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ambao walizaliwa si kwa maumbile ya kibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala mapenzi ya mtu, bali kutokana na Mungu mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao hawakuzaliwa na damu wala na pendo la mwili wa mtu wala na pendo la mwanamume, ila wamezaliwa na Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawakuzaliwa kuwa watoto wa Mungu kwa namna ya kimutu, wala kwa mapenzi ya kimwili, wala kwa mapenzi ya mutu, lakini wamezaliwa na Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.