John 1:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yohane aliwaambia watu habari zake, akasema kwa sauti, “Huyu ndiye niliyemtaja wakati niliposema: ‘Anakuja mtu mmoja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yahya alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yohana alizungumza kuhusu yeye alipopaza sauti na kusema, “Huyu ndiye niliyemzungumzia habari zake niliposema, ‘Anayekuja baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa sababu alikuwepo mwanzoni, zamani kabla sijazaliwa.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yohane aliwaambia watu habari zake, akasema kwa sauti, “Huyu ndiye niliyemtaja wakati niliposema: Anakuja mtu mmoja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yohane aliwaambia watu habari zake, akasema kwa sauti, “Huyu ndiye niliyemtaja wakati niliposema: ‘Anakuja mtu mmoja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yohana alishuhudia habari zake, akapiga kelele akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwako kabla yangu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yahya alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yohane aliwaambia watu habari zake, akasema kwa sauti, “Huyu ndiye niliyemtaja wakati niliposema: ‘Anakuja mtu mmoja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Yohana akamshuhudia yeye na kupaza sauti akisema: Huyu ndiye, niliyemsema: Ajaye nyuma yangu alikuwa mbele yangu, kwani ni mtangulizi wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoane alimushuhudia akisema kwa sauti: “Huyu ndiye niliyesema juu yake: ‘Anayekuja nyuma yangu ananipita, kwa sababu alikuwa mbele sijazaliwa.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yohana akamshuhudia, akapaaza sauti yake, akinena, Huyu ndiye niliyemnena khabari zake, kwamba, Ajae nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.