John 1:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yohane akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nabii Isaya alisema habari zake: ‘Sauti ya mtu anaita jangwani: Nyosheni njia ya Bwana.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yohana akawaambia maneno ya nabii Isaya: “‘Mimi ni mtu anayeipaza sauti yake toka nyikani: Nyoosheni njia kwa ajili ya Bwana.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yohane akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nabii Isaya alisema habari zake: Sauti ya mtu imesikika jangwani: Nyoosheni njia ya Bwana.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yohane akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nabii Isaya alisema habari zake: ‘Sauti ya mtu anaita jangwani: Nyosheni njia ya Bwana.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawajibu kwa maneno ya Nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Inyosheni njia ya Bwana.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yohane akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nabii Isaya alisema habari zake: ‘Sauti ya mtu anaita jangwani: Nyosheni njia ya Bwana.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Ndimi sauti ya mtu apigaye mbiu nyikani: Inyosheni njia ya Bwana, kama alivyosema mfumbuaji Yesaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoane akajibu: “Mimi ni sauti inayotangaza katika jangwa: ‘Munyooshe njia ya Bwana,’ ” sawa vile nabii Isaya alivyosema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Mimi ni sauti ya mtu apaazae sauti jangwani, Inyosheni njia ya Bwana! kama alivyonena nabii Isaya.