John 1:30 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyu ndiye niliyeongea juu yake niliposema: ‘Baada yangu anakuja mtu mmoja aliye mkuu zaidi kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huyu ndiye niliyezungumza habari zake niliposema, “Kuna mtu anayekuja baada yangu aliye mkuu zaidi yangu, kwa sababu yeye aliishi muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwangu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyu ndiye niliyesema juu yake: Baada yangu anakuja mtu mmoja aliye mkuu zaidi kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyu ndiye niliyeongea juu yake niliposema: ‘Baada yangu anakuja mtu mmoja aliye mkuu zaidi kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyu ndiye yule niliyewaambia ya kwamba, ‘Yuaja mtu nyuma yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi kwa maana alikuwako kabla yangu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyu ndiye niliyeongea juu yake niliposema: ‘Baada yangu anakuja mtu mmoja aliye mkuu zaidi kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu ndiye, niliyemsema mimi: Nyuma yangu anakuja mtu aliyekuwa mbele yangu, kwani ni mtangulizi wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyu ndiye niliyesema juu yake kwamba mutu mumoja anakuja nyuma yangu, lakini ananipita kwa sababu alikuwa mbele sijazaliwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Huyu ndiye niliyemnena khabari zake, Yuaja mtu nyuma yangu, aliyekuwa mbele yangu, kwa maana alikuwa kabla yangu.