John 1:39 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawaambia, “Njoni, nanyi mtaona.” Hao wanafunzi wakamfuata, wakaona mahali alipokuwa anakaa, wakashinda naye siku hiyo. Ilikuwa yapata saa kumi jioni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!” Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akajibu, “Njooni tufuatane pamoja nanyi mtapaona ninapokaa.” Hivyo wale watu wawili wakaenda pamoja naye. Wakaona mahali alipokuwa anakaa, nao wakashinda huko pamoja naye mchana wote. Hiyo ilikuwa ni saa kumi ya jioni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawaambia, “Njoni, nanyi mtaona.” Hao wanafunzi wakamfuata, wakaona mahali alipokuwa anakaa, wakashinda naye siku hiyo. Ilikuwa yapata saa kumi jioni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawaambia, “Njoni, nanyi mtaona.” Hao wanafunzi wakamfuata, wakaona mahali alipokuwa anakaa, wakashinda naye siku hiyo. Ilikuwa yapata saa kumi jioni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawajibu, “Njoni, nanyi mtapaona!” Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!” Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Njooni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawaambia, “Njoni, nanyi mtaona.” Hao wanafunzi wakamfuata, wakaona mahali alipokuwa anakaa, wakashinda naye siku hiyo. Ilikuwa yapata saa kumi jioni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawaambia: Njoni, mwone! Basi, wakaja, wakapaona, anapokaa, wakakaa kwake siku ile, ikawa kama saa kumi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akawajibu: “Mukuje na mutaona.” Basi wakaenda, wakaona pahali alipokaa, wakabaki pamoja naye siku ile. (Ilikuwa karibu na saa kumi ya magaribi.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Ilikuwa karibu na saa kumi.