John 1:48 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Nathanaeli akamwuliza, “Umepataje kunijua?” Yesu akamwambia, “Ulipokuwa chini ya mtini, hata kabla Filipo hajakuita, nilikuona.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nathanaeli akamuuliza, “Umenifahamuje?” Isa akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nathanaeli akamwuliza Yesu, “Umenifahamu kwa namna gani?” Yesu akamjibu, “Nilikuona pale ulipokuwa chini ya mtini, kabla Filipo hajakueleza habari zangu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Nathanieli akamwuliza, “Umepataje kunijua?” Yesu akamwambia, “Ulipokuwa chini ya mtini hata kabla Filipo hajakuita, nilikuona.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Nathanaeli akamwuliza, “Umepataje kunijua?” Yesu akamwambia, “Ulipokuwa chini ya mtini, hata kabla Filipo hajakuita, nilikuona.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nathanaeli akamwuliza, “Umenifahamuje?” Yesu akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nathanaeli akamuuliza, “Umenifahamuje?” Isa akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Nathanaeli akamwuliza, “Umepataje kunijua?” Yesu akamwambia, “Ulipokuwa chini ya mtini, hata kabla Filipo hajakuita, nilikuona.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Natanaeli alipomwuliza: Umenitambua tangu lini? Yesu akajibu, akamwambia: Filipo alipokuwa hajakuita bado, ulipokuwa chini ya mkuyu, hapo nimekuona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Natanaeli akamwuliza: “Unanijua namna gani?” Yesu akamujibu: “Filipo alipokuwa hajakuita, nilikuona wakati ulipokuwa chini ya muti wa matunda ya tini.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunijua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwa chini ya mtini, nalikuona.