John 10:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyanganyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang’anyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawaambia, “Hakika ninawaambia, mtu anapoingia katika zizi la kondoo, hutumia mlango. Kama akiingia kwa kutumia njia nyingine yoyote, huyo ni mwizi. Anajaribu kuwaiba kondoo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alisema “Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwivi na mnyang'anyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwizi na mnyang’anyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwizi naye ni mnyang'anyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyanganyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli kweli nawaambiani: Asiyepita mlangoni, apate kuingia zizini mwa kondoo, akipandia pengine, huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akasema: “Kweli, kweli ninawaambia: mutu asiyeingia kwa mulango wa upango wa kondoo, lakini anapandia na kuingilia nafasi ingine, yeye ni mwizi na munyanganyi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
AMIN, amin, nawaambieni, asiyeingia kwa mlango katika zizi la kondoo, lakini apanda penginepo, huyu ni mwizi na mnyangʼanyi.