John 10:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwamwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia, kisha mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Anapomwona mbwa-mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa-mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtumishi anayelipwa ili kuwachunga kondoo yuko tofauti na mchungaji. Mtumishi wa mshahara, kondoo siyo mali yake. Hivyo anapomwona mbwa mwitu anakuja, hukimbia na kuwaacha kondoo peke yao. Mbwa mwitu huwashambulia na kuwatawanya kondoo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwa mwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwamwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia, kisha mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu wa kuajiriwa ambaye kondoo si mali yake, amwonapo mbwa mwitu anakuja, hukimbia na kuwaacha kondoo na mbwa mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Amwonapo mbwa mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwamwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwamwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia, kisha mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mfanya kazi, asiye mchungaji wala mwenye kondoo, huwaacha kondoo na kukimbia anapomwona chui, akija. Naye chui huwakamata na kuwatawanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mutumishi wa mushahara si muchungaji, wala kondoo si wake. Kwa sababu hii wakati anapoona imbwa wa pori anakuja, anaacha kondoo na kukimbia. Na halafu imbwa wa pori anawakamata na kuwasambaza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu wa mshahara, na asiye mchunga, ambae kondoo si mali yake, humwona mbwa wa mwitu anakuja, huziacha kondoo, hukimbia; na mbwa wa mwitu huziteka, huzitawanya.