John 10:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakuna mtu anayeninyanganya uhai wangu; mimi nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu, na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna anayeweza kuuchukua uhai wangu kutoka kwangu. Nautoa uhai wangu kwa hiari yangu. Ninayo haki ya kuutoa, na ninayo haki ya kuuchukua tena. Haya ndiyo aliyoniambia Baba yangu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hakuna mtu anayeninyang'anya uhai wangu; mimi na nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakuna mtu anayeninyang'anya uhai wangu; mimi nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nililipokea kwa Baba yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakuna mtu anayeninyanganya uhai wangu; mimi nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakuna anayenishurutisha hivyo, ila mimi ninajitoa mwenyewe. Nina uwezo wa kujitoa, nife, tena nina uwezo wa kuwapo tena. Hivi ndivyo, alivyoniagiza Baba yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna mutu anayeweza kunionodoa uzima, lakini ninajitoa mwenyewe kufa kwa mapenzi yangu. Niko na uwezo wa kujitoa kufa na niko na uwezo wa kuwa tena muzima. Ni vile Baba yangu alivyoniagiza kufanya.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hakuna mtu aniondoleae, bali mimi nauweka mwenyewe. Nina uweza wa kuuweka, tena nina uweza wa kuutwaa tena. Agizo hili nalilipokea kwa Baba yangu.