John 10:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiwe Kristo, basi, tuambie wazi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wayahudi wakamkusanyikia, wakamuuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka hadi lini? Kama wewe ndiwe Al-Masihi, tuambie waziwazi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Viongozi wa Kiyahudi wakakusanyika kumzunguka. Wakasema, “Ni mpaka lini utatuacha na mashaka juu yako? Kama wewe ndiwe Masihi, basi tuambie wazi wazi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo, basi, tuambie wazi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiwe Kristo, basi, tuambie wazi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wayahudi wakamkusanyikia wakamwuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo tuambie waziwazi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wayahudi wakamkusanyikia wakamuuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiwe Al-Masihi tuambie waziwazi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiwe Kristo, basi, tuambie wazi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wayuda wakamzunguka, wakamwambia: Unatuhangisha roho zetu mpaka lini? Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie waziwazi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Wayuda wakamuzunguka, na kumwambia: “Mpaka wakati gani utatuzungusha kichwa? Kama wewe ni Kristo, utuambie waziwazi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Wayahudi wakamzunguka, wakamwambia, Hatta lini utatuangaisha roho zetu? Kama wewe u Kristo, tuambie wazi wazi.