John 10:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kuwatoa wote nje, yeye hutangulia mbele yao na kondoo humfuata, kwa kuwa wanaijua sauti yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mchungaji huwatoa nje kondoo wake wote. Kisha huwatangulia mbele na kuwaongoza. Kondoo nao humfuata, kwa sababu wanaifahamu sauti yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akisha watoa nje huwatangulia mbele nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akiisha kuwatoa nje hutangulia mbele yao wote walio wake, nao kondoo humfuata, kwani wameijua sauti yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Anapokwisha kuwatia hao kondoo wake inje, anawatangulia, nao wanamufuata kwa sababu wanajua sauti yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Awatoapo nje kondoo zilizo zake, huwatangulia; na kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.