John 10:40 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akaenda tena ngambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akaenda tena ng’ambo ya Yordani hadi mahali Yahya alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akarejea tena kwa kuvuka Mto Yordani hadi sehemu ambapo Yohana alipoanzia kazi ya kubatizia watu. Yesu akakaa huko,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akaenda tena ng'ambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akaenda tena ng'ambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaenda tena ng'ambo ya Mto Yordani mpaka mahali pale ambapo Yohana alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaenda tena ng’ambo ya Mto Yordani mpaka mahali pale ambapo Yahya alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akaenda tena ngambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaondoka tena kwenda ng'ambo ya Yordani mahali pale, Yohana alipokuwa akibatiza hapo kwanza; akakaa pale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaenda zake tena ng’ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yesu akaenda tena ngambo ingine ya Yordani, pahali Yoane alipobatiza watu zamani, na kubaki kule.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaenda zake tena ngʼambu ya Yardani, hatta pahali ptile alipokuwa Yohana akihatiza hapo kwanza; akakaa huko. Watu wengi wakamwendea, wakanena,