John 11:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu mmoja aitwaye Lazaro, mwenyeji wa Bethania, alikuwa mgonjwa. (Kijiji cha Bethania kilikuwa mahali walipokaa Maria na Martha, dada yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mtu mmoja, jina lake Lazaro, alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania, kijiji cha Mariamu na Martha dada yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwepo mtu aliyekuwa mgonjwa aliyeitwa Lazaro. Huyo aliishi katika mji wa Bethania, mahali ambapo Mariamu na dada yake Martha waliishi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu mmoja aitwaye Lazaro, mwenyeji wa Bethania, alikuwa mgonjwa. (Kijiji cha Bethania kilikuwa mahali walipokaa Maria na Martha, dada yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu mmoja aitwaye Lazaro, mwenyeji wa Bethania, alikuwa mgonjwa. (Kijiji cha Bethania kilikuwa mahali walipokaa Maria na Martha, dada yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania kijiji cha Maria na Martha dada zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania kijiji cha Maria na Martha dada zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mtu mmoja alikuwa mgonjwa, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu mmoja aitwaye Lazaro, mwenyeji wa Bethania, alikuwa mgonjwa. (Kijiji cha Bethania kilikuwa mahali walipokaa Maria na Martha, dada yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Kulikuwa na mtu mgonjwa, ndiye Lazaro wa Betania, ni kijiji chao Maria na ndugu yake Marta;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa mutu mumoja aliyeitwa Lazaro, muzaliwa wa Betania aliyepatwa na ugonjwa. Wadada zake Maria na Marta walikaa katika kijiji kile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BASSI mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mtu wa mji wa Mariamu na Martha dada yake.