John 11:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwona ameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Mariamu nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani kwamba alikuwa anaenda kule kaburini kulilia huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wayahudi waliokuwepo nyumbani hapo wakimfariji Mariamu walimwona akiinuka na kuondoka ghafla. Walifikiri alikuwa anaenda kaburini kuomboleza. Hivyo wakamfuata.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwona ameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwona ameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Maria nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani ya kwamba alikuwa anakwenda kule kaburini kulilia huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Maria nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani ya kwamba alikuwa anakwenda kule kaburini kulilia huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alilie huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwona ameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wayuda waliokuwa pamoja naye nyumbani na kumtuliza moyo walipomwona Maria, alivyoinuka upesi na kutoka, wakamfuata wakiwaza, ya kuwa anajiendea kaburini, alie huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wale Wayuda waliokuwa ndani ya nyumba pamoja na Maria kwa kumufariji walipomwona akisimama upesi na kutoka, wakamufuata. Walizani kama anakwenda kulia kwenye kaburi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wale Wayahudi waliokuwa pamoja nae nyumbani, wakimfariji, walipomwona Mariamu, jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, wakamfuata, wakidhani ya kuwa anakwenda kaburini illi alie huko.