John 11:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa na kumwona, alipiga magoti, akamwambia, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mariamu alipofika mahali pale Isa alipokuwa, alipiga magoti miguuni pake na kusema, “Bwana, kama ungekuwa hapa, ndugu yangu hangekufa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mariamu alienda pale Yesu alipokuwa. Naye baada ya kumwona, aliinama miguuni pake Yesu na kusema, “Bwana, kama ungekuwa hapa, kaka yangu asingekufa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa na kumwona, alipiga magoti, akamwabia, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa na kumwona, alipiga magoti, akamwambia, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa, alipiga magoti miguuni Pake na kusema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maria alipofika mahali pale Isa alipokuwa, alipiga magoti miguuni pake na kusema, “Bwana Isa, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa na kumwona, alipiga magoti, akamwambia, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maria alipofika hapo, Yesu alipokuwa, akamwangukia miguuni alipokwisha kumwona, akamwambia: Bwana, kama ungalikuwapo hapa, umbu langu hangalikufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maria alipofika pale Yesu alipokuwa na kumwona, akaanguka kwenye miguu yake na kusema: “Bwana, kama ungekuwa hapa, kaka yangu hangekufa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Mariamu, alipofika pale alipokuwapo Yesu, akamwona, akaanguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungaliwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa.