John 11:33 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye wanalia pia, alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipomwona Mariamu akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Isa alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo Yesu alipomwona Mariamu na watu waliokuwa pamoja naye wakilia, akahuzunika na kusikitika sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye wanalia pia, alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye wanalia pia, alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alipomwona Maria akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Yesu alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipomwona Maria akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Isa alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye wanalia pia, alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu alipoona, anavyolia, nao Wayuda waliokuja pamoja naye wanavyolia nao, akachemka rohoni, akajisisimua,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Yesu alipomwona akilia, na wale Wayuda waliokuja pamoja naye wakilia vilevile, akasisimua kwa huzuni nyingi na kufazaika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana nae wanalia, akaugua rohoni, akajifadhaisha nafsi yake,