John 11:44 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo aliyekuwa amekufa akatoka nje, huku amefungwa sanda miguu na mikono, na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia, “Mfungueni, mkamwache aende zake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Isa akawaambia, “Mfungueni; mwacheni aende zake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yule mtu aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono na miguu yake ilikuwa imefungwa sanda. Uso wake ulikuwa umefunikwa kwa kitambaa. Yesu akawaambia watu, “Mfungueni hizo sanda na kumwacha aende.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo aliyekuwa amekufa akatoka nje, huku amefungwa sanda miguu na mikono, na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia, “Mfungueni, mkamwache aende zake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo aliyekuwa amekufa akatoka nje, huku amefungwa sanda miguu na mikono, na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia, “Mfungueni, mkamwache aende zake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Yesu akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Isa akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatoka nje yule aliyekufa, akiwa amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo aliyekuwa amekufa akatoka nje, huku amefungwa sanda miguu na mikono, na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia, “Mfungueni, mkamwache aende zake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, yule aliyekufa alipotoka nje hivyo, alivyokuwa amefungwa kwa sanda miguu na mikono, nao uso wake ulikuwa umefunikwa kwa mharuma. Yesu akawaambia: Mfungueni, mmwache, aende zake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu yule marehemu akatoka inje, akiwa amefungwa mikono na miguu kwa vitambaa, na uso wake ukifunikwa na nguo. Yesu akawaambia: “Mumufungue, mumwache ajiendee.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa saanda miguuni na mikononi, na uso wake umefungwa kitambaa. Yesu akawaambia, Mfungueni, kamwacheni aende zake.