John 11:47 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo makuhani wakuu na Mafarisayo wakafanya kikao cha Baraza Kuu, wakasema, “Tufanye nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa Baraza la Wayahudi. Wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaitisha kikao cha baraza kuu. Wakasema, “Tutafanyaje? Mtu huyu anafanya ishara nyingi sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
kwa hiyo makuhani wakuu na Mafarisayo wakafanya kikao cha Baraza kuu, wakasema, “Tufanye nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo makuhani wakuu na Mafarisayo wakafanya kikao cha Baraza Kuu, wakasema, “Tufanye nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa baraza, wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa baraza. Wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo makuhani wakuu na Mafarisayo wakafanya kikao cha Baraza Kuu, wakasema, “Tufanye nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Ndipo, watambikaji wakuu na Mafariseo walipoikusanya baraza ya wakuu wote, wakasema: Tufanyeje? Kwani mtu huyu anafanya vielekezo vingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wakubwa wa makuhani na Wafarisayo wakakusanya Baraza yao Kubwa, na kusema: “Tufanye nini kwa kuona mutu huyu anaonyesha vitambulisho vingi?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi makuhani wakuu na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakanena, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.