John 11:51 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye hakusema hivyo kwa hiari yake mwenyewe, bali kwa vile alikuwa kuhani mkuu mwaka huo, alibashiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lao;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe, bali kama kuhani mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Isa angekufa kwa ajili ya taifa la Wayahudi;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kayafa hakufikiri hivi peke yake. Hakika kama kuhani mkuu kwa mwaka ule, alikuwa akitabiri kwamba Yesu angekufa kwa ajili ya Wayahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye hakusema hivyo kwa hiari yake mwenyewe, bali kwa vile alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo, alibashiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye hakusema hivyo kwa hiari yake mwenyewe, bali kwa vile alikuwa kuhani mkuu mwaka huo, alibashiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lao;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama Kuhani Mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Yesu angelikufa kwa ajili ya Wayahudi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Isa angelikufa kwa ajili ya taifa la Wayahudi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye hakusema hivyo kwa hiari yake mwenyewe, bali kwa vile alikuwa kuhani mkuu mwaka huo, alibashiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lao;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini neno hili hakulisema kwa mawazo yake, ila kwa kuwa alikuwa mtambikaji mkuu wa mwaka ule, alifumbua yajayo, kwani Yesu alitumwa afe kwa ajili ya kabila lote;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
(Yeye hakusema maneno haya kutokana na mawazo yake mwenyewe; lakini kwa maana yeye ndiye aliyekuwa Kuhani Mukubwa mwaka ule, alitabiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa la Wayuda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na hili hakusema kwa nafsi yake, hali kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lile;