John 11:52 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na wala si kwa ajili yao tu, bali pia apate kuwaleta pamoja watoto wa Mungu waliotawanyika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wala si kwa ajili ya taifa hilo pekee, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kweli, angekufa kwa ajili ya Wayahudi. Lakini pia angekufa kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika ulimwenguni pote. Angekufa ili awakusanye na kuwaweka katika kundi moja.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na wala si kwa ajili yao tu, bali pia apate kuwaleta pamoja watoto wa Mungu waliotawanyika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na wala si kwa ajili yao tu, bali pia apate kuwaleta pamoja watoto wa Mungu waliotawanyika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wala si kwa ajili ya Wayahudi peke yao, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wala si kwa ajili ya taifa hilo pekee, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na wala si kwa ajili yao tu, bali pia apate kuwaleta pamoja watoto wa Mungu waliotawanyika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini siko kufa kwa ajili ya kabila lake tu, ila ni kwamba, apate kuwakusanya pamoja nao watoto wa Mungu waliotawanyika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kufa kwake si kwa ajili ya taifa hili tu, lakini vilevile kwa ajili ya watoto wa Mungu waliosambazwa, kusudi apate kuwaunga katika umoja.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wala si kwa ajili ya taifa lile tu, lakini pamoja na haya awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika wawe wamoja.