John 11:54 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, Yesu hakutembea tena hadharani kati ya Wayahudi, bali alitoka hapo, akaenda mahali karibu na jangwa, katika mji uitwao Efraimu. Akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Isa akawa hatembei tena hadharani miongoni mwa Wayahudi, bali alijitenga akaenda sehemu iliyo karibu na jangwa kwenye kijiji kiitwacho Efraimu. Akakaa huko na wanafunzi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo Yesu akaacha kusafiri wazi wazi katikati ya Wayahudi. Akaelekea katika mji ulioitwa Efraimu uliokuwa kwenye eneo karibu na jangwa. Akakaa huko pamoja na wafuasi wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo, Yesu hakutembea tena hadharani kati ya Wayahudi, bali alitoka hapo, akaenda mahali karibu na jangwa, katika mji uitwao Efraimu. Akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, Yesu hakutembea tena hadharani kati ya Wayahudi, bali alitoka hapo, akaenda mahali karibu na jangwa, katika mji uitwao Efraimu. Akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Yesu akawa hatembei hadharani miongoni mwa Wayahudi, bali alijitenga akaenda sehemu iliyo karibu na jangwa kwenye kijiji kiitwacho Efraimu. Akakaa huko na wanafunzi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Isa akawa hatembei hadharani miongoni mwa Wayahudi, bali alijitenga akaenda sehemu iliyo karibu na jangwa kwenye kijiji kiitwacho Efraimu. Akakaa huko na wanafunzi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, Yesu hakutembea tena hadharani kati ya Wayahudi, bali alitoka hapo, akaenda mahali karibu na jangwa, katika mji uitwao Efraimu. Akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yesu hakutembea tena waziwazi kwa Wayuda, ila akaondoka kule, akaenda katika nchi iliyokuwa karibu ya nyikani, akaingia mji uitwao Efuraimu. Mle akakaa pamoja na wanafunzi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hii Yesu hakutembea tena akijionyesha waziwazi kati ya Wayuda. Kisha akajiendea pamoja na wanafunzi wake katika inchi iliyokuwa karibu na jangwa katika muji unaoitwa Efuraimu. Nao wakabaki kule.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Yesu hakutemhea tena kwa wazi kati ya Wayahudi, hali alitoka huko akaenda mahali karibu ya jangwa, hatta mji nitwao Efraim; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.