John 12:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaza sauti wakisema: “Sifa! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!” “Amebarikiwa mfalme wa Israeli!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hawa walibeba matawi ya miti ya mitende na kwenda kumlaki Yesu. Pia walipiga kelele wakisema, “‘Msifuni Yeye!’ ‘Karibu! Mungu ambariki yeye ajaye kwa jina la Bwana!’ Mungu ambariki Mfalme wa Israeli!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaaza sauti wakisema: “Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaza sauti wakisema: “Sifa! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana Mwenyezi Mungu!” “Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaza sauti wakisema: “Sifa! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakachukua makuti ya mitende, wakatoka kumwendea, wakapaza sauti: Hosiana! Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana! Ndiye mfalme wa Isiraeli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wakatwaa matawi ya ngazi na kwenda kumupokea, wakilalamika kwa sauti kubwa, wakisema: “Mungu asifiwe! Abarikiwe huyu anayekuja kwa jina la Bwana! Abarikiwe mufalme wa Waisraeli!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakatwaa matawi ya mitende wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana; Amebarikiwa ajiie kwa jina la Bwana, mfalme wa Israeli.