John 12:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kundi la watu wale waliokuwa pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua kutoka kwa wafu, walimshuhudia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale waliokuwepo Isa alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu waliendelea kushuhudia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku Yesu alipomfufua Lazaro kutoka wafu na kumwambia atoke kaburini walikuwepo watu wengi pamoja naye. Hawa walikuwa wakiwaeleza wengine yale aliyoyafanya Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kundi la watu wale waliokuwa pamoja naye wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua kutoka wafu, walisema yaliyotukia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kundi la watu wale waliokuwa pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua kutoka kwa wafu, walimshuhudia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale waliokuwepo wakati Yesu alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu, waliendelea kushuhudia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale waliokuwepo wakati Isa alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu, waliendelea kushuhudia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kundi la watu wale waliokuwa pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua kutoka kwa wafu, walimshuhudia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata wale watu wengi waliokuwa pamoja naye, alipomfufua Lazaro katika wafu na kumwita, atoke kaburini, wakavishuhudia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watu wote waliokuwa pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro toka ndani ya kaburi na kumufufua walishuhudia mambo yaliyofanyika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wakamshuhudia makutano waliokuwa pamoja nae alipomwita Lazaro kutoka kaburini akamfufua.