John 12:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wameenda kuabudu wakati wa Sikukuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hapo Yerusalemu walikuwepo pia Wayunani. Hawa walikuwa ni miongoni mwa watu walioenda mjini humo kuabudu wakati wa sikukuu ya Pasaka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi palikuwapo Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wamekwenda kuabudu wakati wa Sikukuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wamekwenda kuabudu wakati wa Sikukuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Palikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Miongoni mwao waliopanda kutambika siku za ile sikukuu mlikuwa na Wagriki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa Wagriki wamoja kati ya wale watu waliofika Yerusalema kuabudu wakati wa sikukuu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliopanda kwenda kuabudu wakati wa siku kuu.