John 12:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: ‘Baba, usiruhusu saa hii inifikie?’ Lakini ndiyo maana nimekuja — ili nipite katika saa hii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii’? Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa ninapata taabu sana rohoni mwangu. Nisemeje? Je, niseme, ‘Baba niokoe katika wakati huu wa mateso’? Hapana, nimeufikia wakati huu ili nipate mateso.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: Baba, usiruhusu saa hii inifikie? Lakini ndiyo maana nimekuja—ili nipite katika saa hii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: ‘Baba, usiruhusu saa hii inifikie?’ Lakini ndiyo maana nimekuja — ili nipite katika saa hii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe na saa hii.’ Lakini, ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii.’ Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: ‘Baba, usiruhusu saa hii inifikie?’ Lakini ndiyo maana nimekuja – ili nipite katika saa hii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa roho yangu imezizimka, nami nisemeje? Niseme: Baba, uniokoe, nisiifikie saa hiyo? Lakini kwa sababu hiyo nimeijia saa hiyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Sasa roho yangu inafazaika. Nami sijui niseme nini. Nimwombe Baba, aniokoe toka mambo yale yatakayofika saa hii? Hapana, kwa sababu nimefika kwa ajili ya yale yatakayofanyika saa hii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sasa roho yangu imefadhaika; niseme nini? Baba, uniokoe na saa hii. Lakini kwa ajili ya hayo naliifikia saa hii. Baba, ulitukuze jina lako.