John 12:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umati ule wa watu wakapaza sauti, wakasema, “Tumesikia kutoka Torati kwamba Al-Masihi adumu milele; hivyo wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu’? Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wakasema, “Lakini sheria yetu inasema kwamba Masihi ataishi milele. Sasa kwa nini unasema, ‘Ni lazima Mwana wa Adamu ainuliwe juu’? Ni nani huyu ‘Mwana wa Adamu’?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na Sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ule umati wa watu ukapiga kelele ukasema, “Tumesikia kutoka katika Torati kwamba ‘Kristo adumu milele,’ wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu?’ Huyu ‘Mwana wa Adamu ni nani?’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ule umati wa watu ukapiga kelele, ukasema, “Tumesikia kutoka Torati kwamba ‘Al-Masihi adumu milele.’ Wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu?’ Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wakamjibu: Sisi tumesikia katika Maonyo: Kristo atakaa kale na kale; tena inakuwaje, wewe ukisema: Mwana wa mtu sharti akwezwe juu? Huyo Mwana wa mtu ni nani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na lile kundi la watu wakamujibu: “Sisi tumesikia katika maandiko ya Sheria kwamba Kristo ataishi milele. Basi namna gani unaweza kusema kama Mwana wa Mutu anapaswa kunyanyuliwa juu? Na huyu Mwana wa Mutu ni nani?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi makutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hatta milele: nawe wanenaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?