John 12:40 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Amewafanya vipofu, na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka nami nikawaponya.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Mungu aliwafanya baadhi ya watu wasione. Aliufunga ufahamu wao. Alifanya hivi ili wasiweze kuona kwa macho yao na kuelewa kwa ufahamu wao. Alifanya hivyo ili wasiweze kugeuka na kuponywa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Amewafanya vipofu na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka, nami nikawaponya.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Amewafanya vipofu, na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka nami nikawaponya.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amewapofua macho, akaishupaza mioyo yao, wasije wakaona kwa macho yao, au wakajua maana kwa mioyo yao, au wakageuka, nami nikawaponya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mungu amepofusha macho yao, kusudi yasipate kuona. Ameifanya mioyo yao kuwa migumu, wala wasipate kunigeukia nami ningewaponyesha.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Amewapofusba macho, amefanya migumu mioyo yao, Wasije wakaona kwa macho yao, wakafahamu kwa mioyo yao, Wakagenka, nikawaponya.