John 12:48 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: Neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yuko anayehukumu yule anayenikataa mimi na kuyakataa maneno yangu; yale maneno niliyoyasema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Isipokuwa yupo hakimu wa kuwahukumu wote wanaokataa kuniamini na wasiokubaliana na yale ninayoyasema. Ujumbe ninaousema utawahukumu ninyi siku ya mwisho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: Neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Anikataaye, asiyapokee maneno yangu, anaye atakayemhukumu. Neno, nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule anayenikataa na asiyekubali maneno yangu atahukumiwa kufuatana nayo. Ni lile neno nililosema ndilo litakalomuhukumu siku ya mwisho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.